Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: “Ayatulla Sheikh Isa Qasim” ambaye siku kadhaa ziliopita alinyang`anywa utaifa wake nchini Bahrain kutoka kwa utawala wa nchini hiyo almesema: kamwe sitatafuta suluhu na utawala wa Ali Khalifa kwa kutoka nchini Bahrain.
Baada ya kunyang`anywa urai wa mwanazuoni huyo wa Bahrain, hatua ambayo kimefanywa kinyume na sheria hata za kimataifa, serikali ya nchi hiyo inaendelea kufanya shinikizo la kumwondosha mwanazuoni huyo katika nchi yake, ama wananchi wa nchi hiyo wameamuamua kukusanyika na kuizunguka nyumba ya mwanazuoni huyo kwa muda wote katika mji mkuu wa nchi hiyo, huku wakisisitiza kuwa endapo serikali itaamua kutumia njia yeyote ya ukatili katika kumkamata mwanazuoni huyo, wao watakuwa tayari kwa lolote hata kwa kumwaga damu.
“Sheikh Abdulaah Aldaqaq” mmoja kati ya wanaharakati wa Bahrain pia amesisitiza katika suala hilo na kusema kuwa:kumwondoa Ayatulla Sheikh Isa Qasim katika nchi ya Bahrain kutaifanya nchi hiyo kuingia katika majanga na kukosa amani.
Harakati ya mapinduzi ya wananchi wa Bahrain yameanza tarehe 14 mwezi wa pili mwa 2011 na mpaka sasa mamia ya wananchi wa nchi hiyo wameuwawa, kujeruhiwa na kufungwa.
Ama katika miezi ya hivi karibuni serikali ya nchi hiyo imeongoza kuwa wanchi hao kwa sura mpya, hatua mpya hiyo ilianza kuonekana baada ya kikao kilichofanyika na viongozi wa ulinzi wa serikali ya Ali Khalifa ambapo katika kikao hicho walikubaliana kulimaliza suala la mapinduzi ya 2011 nchini humo.
Kwa mujibu ripoti za kikao hicho, viongozi wa usalama wa Bahrain wametishia kuwa kuanzia tarehe 15 ya mwezi juni mwaka huu itaanza hatua mpya. Katika hatua kunashuhudiwa vita mpya ya serikali ya Bahrain na asilimia kubwa ya wananchi wa hiyo ambao ni wafuasi wa dhehebu la Shia, ambapo hatua ya kwanza kukifunga cha kikubwa cha kisiasa nchini humo cha (Alwefaq) pia kuviengua jumuia mpili za kidini nchini humo, pia kumkama kwa mara ya pili mwanaharakati “Nabil Rajab” na kuwanyang`anya uraia baadhi ya wanazuoni na wanaharaki mashuhuri ikiwemo Ayatulla Sheikh Isa Qasim na kutishia kumtoa kwa nguvu katika nchi hiyo.
mwisho wa Habari/290